Thursday, February 10, 2011

MWISHO WA DUNIA



SIKU YA HUKUMU!
Mei 21, 2011

hourglass
Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge aumapo mwanadamu.Ufunuo 9:5

MWISHO WA DUNIA
OKTOBA 21, 2011


Lengo la kiperushi hiki ni kukuarifu juu ya uharaka mkubwa uliopo sasa duniani kwa kila mtu kupatana na Mungu. Biblia ni Neno la Mungu! Kila kitu Biblia inatamka kinamamlaka kamili ya Mungu Mwenyewe. Sasa, wakati huu Biblia inatupa habari ambayo dhahiri kabisa inafunua mpango wa Mungu juu ya siku ya hukumu na mwisho wa dunia yenyewe. Biblia imeshafunua siri zake juu ya nyakati za historia. Habari hii haikufahamika kamwe hapo mbeleni kwa sababu Mungu Alilifunga Neno Lake Akizuia kila jaribio la kupata ufahamu wa mwisho wa dunia. Tunasoma juu ya hili katika kitabu cha Danieli:
Daniel 12:9 Akasema, Enenda zako, Daniel; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho.
Hata hivyo, katika wakati huu wa sasa, Mungu Amelifungua Neno Lake (Biblia ) ili kufunua kiwango kikubwa cha ukweli kuhusu mwisho wa wakati (pamoja na mafundisho mengine mengi) Sura ile ile katika Danieli, inasema:
Daniel 12:4 Lakini wewe, Ee Daniel, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Mungu sasa Analifungua Neno Lake kwa sababu tumefika wakati wa mwisho. Kwa sababu hii, imekuwa wazi kabisa kwa mwanafunzi wa Biblia aliye makini kwamba sasa tunaishi katika siku chache za mwisho wa historia ya dunia.Kwa kweli, kwa sababu tunaishi katika mwisho wa wakati, Mungu sasa anawafunulia watu Wake habari ifuatayo:

KALENDA YA KIBIBLIA YA HISTORIA

Bwana amefungua ufahamu wa watu wake wa “kalenda ya kibiblia” ipatikanayo katika kurasa za Biblia.Simulizi uzao za kitabu cha Mwanzo, hasa sura za 5 na 11, zinaweza kuonyeshwa kuwa ni kalenda ya historia ya mwanadamu katika dunia hii. Kalenda ya historia ya Biblia iko sahihi kabisa na ni ya kuaminika. Kwa kuwa kalenda hii imetolewa na Mungu katika Neno Lake, inaweza kuaminiwa kwa moyo wote. Katika kipeperushi hiki kifupi tutakushirikisha baadhi ya mahitimisho yaliyotoka katika kalenda ya ki-Biblia na mafundisho mengine katika Maandiko.
Hata hivyo, kiwango cha habari kilochopo ni kikubwa sana na vigumu kuweza kuelezewa kwa undani katika kipeperushi hiki kifupi; tunaweza na tutakupa tarehe za uhakika na za kuaminika. Tarehi hizi zinaweza kuaminika kabisa kwa sababu zinatoka katika Biblia. (EBiblefellowship haina ushirika na Family Radio; hata hivyo, tunakushauri upate nakala yako ya bure ya kitabu “We Are Almost There” kwa kuwaandikia kupitia anuani ifuatayo: Family Stations Inc, Hegenberger Rd.,Oakland,CA 94621. Kitabu hiki kinaeleza kwa kina juu ya wakati wa siku ya Hukumu na mwisho wa dunia. Pia waweza kukisoma au kukinakili toka katika mtandao: www.familyradio.com).

UTOKEAJI WA MATUKIO MUHIMU KATIKA HISTORIA

11,013 K.K—Uumbaji. Mungu Aliiumba dunia na mtu (Adamu na Hawa).
4990 K.K—Gharika ya siku ya Nuhu. Wote waliangamia katika mafuriko ya dunia nzima. Nuhu pekee, mke wake, na watoto wake watatu wakiume na wake zao walinusurika katika safina (miaka 6023) baada ya uumbaji).
7 K.K—Mwaka aliozaliwa Yesu Kristo (miaka 11,006 baada ya uumbaji).
33 B.K—Mwaka aliosulibiwa Yesu Kristo na mwanzo wa enzi ya kanisa (miaka 11,045 baada ya uumbaji).
1988 B.K—Mwaka huu enzi ya kanisa iliisha na kipindi cha miaka 23 ya dhiki kuu ikaanza (miaka 13,000 baada ya uumbaji).
1994 B.K—Tarehe 7 Septemba, siku 2300 za kipindi cha kwanza cha dhiki kuu kiliisha na mvua za vuli zikaanza, kuanzisha mpango wa Mungu kuuokoa umati mkubwa wa watu nje ya makanisa (miaka 13,006 baada ya uumbaji).
2011 B.K—Tarehe 21 Mei, siku ya Hukumu itaanza na unyakuo (kutwaliwa kwa wateule wa Mungu kwenda mbinguni) utatokea mwishoni mwa miaka 23 ya dhiki kuu. Tarehe 21 Oktoba, 2011 dunia itaangamizwa kwa moto (miaka 7000 baada ya gharika; miaka 13,023 baada ya uumbaji).

SIKU MOJA NI KAMA MIAKA 1000

Mtoto wa Mungu amejifunza na kuelewa katika Biblia kwamba lugha iliyotumika katika Mwanzo sura ya 7 ina maana mbili:
Mwanzo 7:4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Kihistoria, Mungu Aliponena maneno haya, zilikuwa zimebaki siku saba kwa Nuhu, nyumba yake, na wanyama kuingia na kuwa salama katika safina; kiroho (Biblia ni kitabu cha kiroho), Mungu Alikuwa Anawaambia wanadamu wote duniani kwamba mwandamu muovu ana miaka 7,000 kutafuta usalama katika wokovu uliotolewa na Yesu Kristo. Tunawezaje kujua hili? Tunajua hivi ndivyo inamaanisha kwa sababu ya 2 Petro 3 inavyosema:
2 Petro 3:6-8 Kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikalindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
Mazingira ya 2 Petro ni ya muhimu sana! Katika mistari michache ya kwanza, Mungu Anatupeleka katika kuharibiwa kwa dunia enzi za Nuhu.Kisha tunaonywa kwamba tusiwe “wajinga” wa jambo moja, nalo ni, siku 1 ni kama miaka 1,000, na miaka 1,000 ni kama siku 1. Mara tu baada ya dokezo hili ni maelezo waziwazi ju ya mwisho wa dunia hii iliyopo kwa moto.
Je, Mungu Atakua Anatuambia nini kwa kulinganisha siku 1 na miaka 1,000?
Kwa kuwa tumegundua hivi karibuni katika Biblia kalenda ya Historia, tunaona kwamba gharika ya Nuhu ilitokea mwaka 4990 K.K. Tarehe hii ni sahihi kabisa (Kwa maelezo zaidi juu ya nyakati za kihistoria kibiblia, tafadhali fungua mtandao wa: www.familyradio.com).  Ilikuwa mwaka 4990 K.K ambapo Mungu Alimfunulia Nuhu kwamba kutakuwa na siku 7 kabla gharika ya maji haijaifunika dunia. Sasa, tukiifanya miaka 1,000 kuwa badala ya kila siku moja ya zile siku 7, tunapata miaka 7,000. Na tukihesabu miaka 7,000 toka gharika ya Nuhu tunapata mwaka 2011 B.K.
   4990 + 2011 = 7001   
Angalizo: Tukihesabu toka miaka ya Agano la kale kwenda Agano jipya, lazima tutoe mwaka mmoja kwa sababu hakuna mwaka sifuri:
   4990 + 2011 – 1 = 7000 kamili.
Mwaka 2011 B.K utakuwa mwaka wa 7,000 baada ya gharika ya Nuhu. Utakuwa ndio mwisho wa muda aliopewa mwanandamu kupata rehema machoni pa Mungu. Hii inamaanisha kwamba muda wa kupata usalama katika Kristo umebaki kidogo mno. Zimebaki siku chache tu kabla 2011 B.K kufika!
Si jambo la kushangaza kwamba watoto wa Mungu wamepewa ufahamu wa mwisho wa dunia. Kimsingi, Biblia inasema hii ni kawaida.Hapo zamani, Mungu Aliwanonya watu Wake juu ya ujio wa vipindi vya hukumu:
Amos 3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri zake.
Waebrania 11:7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani

SIKU YA HUKUMU: 21 MEI 2011

Tunajua kwamba mwaka 2011 ni mwaka wa 7,000 baada ya gharika. Tunajua pia kwamba Mungu Ataingamiza dunia hii mwaka huo. Lakini ni wakati gani hasa wa 2011 hili litatokea?
Jibu linasisimua. Hebu tuangalie gharika kwa maana nyingine katika kitabu cha Mwanzo:
Mwanzo 7:11 IKatika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile ile chemchem zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguliwa.
Mungu ni Mwaminifu kwa Neno Lake na Aliileta gharika siku 7 baadaye katika mwaka wa 6,000, siku ya 17 ya mwezi wa 2 wa kalenda inayohesabiwa kutokana na siku za maisha ya Nuhu. Ilikuwa katika siku hii ya 17 ya Mwezi wa pili ambapo Mungu alifunga mlango wa safina, akihakikisha usalama wa wote waliokuwa ndani na mustakbala wa wote waliokuwa duniani nje ya safina. Kwa hakika wote wameangamia katika maangamizi ya dunia nzima.
Mwanzo 7:16,17 Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia. Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi.
Hapo juu kidogo imeelezwa enzi ya kanisa ilikwisha mwaka 1988 B.K. Ilitokea kwamba enzi ya kanisa ilianza katika siku ya Pentekoste (Mei 22) katika mwaka 33 B.K Halafu miaka 1955 baadaye, enzi ya kanisa ilifikia tamati tarehe 21 Mei, siku ya pentekoste 1988.
Biblia inafundisha kwamba mwisho wa enzi ya kanisa umekuja sambamba na mwanzo wa dhiki kuu:
Mathayo 24:21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
Tarehe 21 Mei 1988, Mungu Aliacha kuyatumia makanisa na madhehebu ya duniani. Roho wa Mungu Aliyaacha makanisa yote na Shetani, mwana wa uasi, akaingia katika makanisa kutawala kuanzia wakati huo.Biblia inafundisha kuwa kipindi hiki cha hukumu juu ya makanisa kitachukua miaka 23 kamili (siku 8,400) kuanzia Mei 21 1988 mpaka Mei 21, 2011.
Habari hizi zimegunduliwa katika Biblia tofauti kabisa na habari kuhusu miaka 7,000 baadada ya gharika. Kwa hiyo tunaona miaka 23 kamili ya kipindi cha dhiki kuu inaishia Mei 21, 2011. Siku hii ndio siku haswa ambayo dhiki kuu itakwisha, na uwezekano mkubwa kwamba hii ndiyo siku ya mwisho ya miaka 7,000 tokea gharika ya Nuhu.
Kumbuka kwamba Mungu Aliufunga mlango wa safina siku ya 17 ya mwezi wa 2 wa kalenda ya Nuhu. Tunaona pia kwamba Mei 21, 2011 ni mwisho wa kipindi cha dhiki kuu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya mwezi wa 2 na siku ya 17 ya kalenda ya Nugu na Mei 21, 2011 ya kalenda yetu ya Kigregoria. Uhusiano huu hauwezi kuonekana waziwazi mpaka tugundue kuwa kuna kalenda nyingine ambayo lazima tuiangalie, ambayo ni kalenda ya kiyahudi ( au ya ki-Biblia). Mei 21, 2011 ni sawa na siku ya 17 ya mwezi wa 2 ya kalenda ya kiyahudi. Kwa hili, Mungu anatuhakikishia kuwa tumeelewa kwa usahihi miaka 7,000 toka gharika. Mei 21, 2011 ni tarehe sambamba na tarehe ambayo Mungu Aliufunga mlango wa safina ya Nuhu. Kwa uelewa huu, pamoja na habari zingine kutoka katika Biblia, tunaona kuwa Mei 21, 2011 itakuwa ndiyo siku ambayo Mungu atawachukua wateule Wake kwenda mbinguni. Mei 21, 2011 itakuwa siku ya hukumu! Hii ndiyo siku Mungu Atafunga mlango wa wokovu kwa dunia.
Kwa maneno mengine, mwisho wa dhiki kuu kuishia siku ambayo ni sambamba na siku ya 17 ya mwezi wa 2 wa kalenda ya Nuhu, bila shaka inatuhakikishia kuwa hii ndiyo siku ambayo Mungu amepanga kuufunga milele mlango wa kuingia mbinguni:
Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Biblia iko wazi kabisa kwamba Kristo ndiye njia pekee ya kwenda mbinguni. Yeye pekee ndiye mlango wa kuingia Ufalme Wake wa mbinguni:
Matendo ya Mitume 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mara baada ya mlango (Yesu) kufungwa siku ya Hukumu, hakuna tena uwezekano wa wokovu hapa duniani:
Ufunuo 3:7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
Biblia inafundisha kwamba, Mei 21, 2011, waumini wa kweli pekee walioteuliwa kupokea wokovu watanyakuliwa toka ulimwengu huu kumpokea Bwana mawinguni na kuwa na Bwana milele:
1 Wathesalonike 4:16,17 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Wanadamu wote waliosalia (mabilioni ya watu) wataachwa katika hukumu ya Mungu, kipindi cha miezi mitano ya mateso ya kutisha hapa duniani:
Ufunuo 9:3-5 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya mungu katika vipaji vya nyuso zao. Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

MWISHO WA DUNIA: OKTOBA 21, 2011

Kwa neema na rehema za Mungu za ajabu, Ametupa onyo juu ya kile Anachotaka kukifanya. Katika siku ya hukumu, Mei 21, 2011, kipindi hiki cha miezi mitano ya mateso ya kutisha kwa wakazi wote wa duniani kitaanza. Mei 21, 2011 ndiyo siku ambayo Mungu Atawafufua wafu wote toka makaburini mwao. Matetemeko ya ardhi yataiharibu dunia na ardhi haitawazuia tena wafu wake (Isaya 26:21). Miili ya watu waliokufa wakiwa wameokoka itafufuliwa na kisha wataondoka mara moja kwenda kuwa na Bwana milele. Wale waliokufa hawajaokoka, watafufuliwa pia lakini miili yao isiyo na uhai itazagaa juu ya uso wa nchi yote. Kifo kitakuwa kila mahali:
Mwanzo 7:24 Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
Miezi mitano baada ya Mei 21, 2011, itakuwa Oktoba 21, 2011. Imetokea pia kuwa Oktoba 21 ya 2011 ni siku ya mwisho ya sikukuu ya vibanda (husherehekewa sambamba na sikukuu ya kukusanya) Sikukuu ya vibanda husherehekewa katika mwezi wa 7 wa kalenda ya kiebrania. Namna ambayo Mungu anaiongelea sikukuu hii katika Biblia ni muhimu sana:
Kutoka 23:16 …tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani.
Kutoka 34:22 Nawe utaitunza sikukuu ya majuma, nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka.
Sikukuu ya vibanda/kukusanya ilisherehekewa “mwisho wa mwaka” hata kama ilkuwa ni mwezi wa 7 kiebrania ambao sio mwisho wa mwaka. Hii ni kwa sababu, kiroho, kutimia kwa sikukuu hii ni mwisho wa dunia. Tarehe 21 oktoba, 2011 itakuwa mwisho wa sikukuu ya vibanda na ya mwisho wa dunia hii. Biblia inaeleza nini kitatokea Oktoba 21, 2011 katika mistari ifuatayo:
2 Petro 3:10 Lakini siku ya bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Sambamba na dunia na ulimwengu, wote ambao wametenda dhambi dhidiya Mungu na hawakunyakuliwa wataangamizwa na moto huu na hawatakuwapo milele:
2 Wathesalonike 1:8,9 katika mwali wa moto; huku akiwalipizia kisasi wao wasiomjua mungu, na wao wasioitii injili ya Bwana wetu yesu; Watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
Tarehe 21 Oktoba, 2011, Mungu atauangamiza kabisa uumbaji huu pamoja na watu wote ambao hawakukokolewa na Yesu Kristo. Malipo ya kutisha kwa ajili ya uasi wao dhidi ya Mungu yatakamilishwa kwa wao kupoteza uzima wa milele. Wapendwa hawa watakoma kabisa kuwapo kuanzia 21 Oktoba 2011. Inasasikitisha kiasi gani kwamba mwanadamu mstahiki, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu atakufa kama mnyama na kuangamia milele:
Zaburi 49:12 Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, bali amefanana na wanyama wapoteao.
Kuna mengi ya kuongea, lakini mpendwa hili ni onyo kwa nafsi wewe kwamba muda wa wokovu unakaribia kwisha! Mungu Aliupa ulimwengu miaka 7,000 kutoka gharika, na sasa siku chache tu zimebaki kufikia Mei 21, 2011. Kufumba na kufumbua, muda utakuwa umekwisha. Mchanga kidogo uliobaki katika glasi ya saa utakuwa umeisha na hautakuwapo milele. Ingawa muda kidogo tu umebaki, tumaini la wokovu kwa mtu yeyote bado lipo leo:
2 Wakorintho 6:2 (Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa;)
Haimchukui Mungu muda mrefu kumuokoa mtu.katika masaa ya mwisho ya maisha ya dhambi , Kristo alimuokoa mwivi msalabani:
Luka 23:42,43 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa nami peponi.
Maombi yetu ni kwamba utakipokea kipeperushi hiki kwa moyo wa kujali kabisa kama jinsi kilivyotolewa. Usomapo, tafadhali zingatia mistari toka katika Biblia kwa sababu ni Neno la Mungu na kwa hiyo lina nguvu na mamlaka kamili. Tumaini letu pekee la wokovu ni kupitia kusikia Neno la Mungu. Leo mlango wa mbinguni upo wazi. Sasa ndio wakati Mungu anaokoa umati mkubwa wa watu toka ulimwenguni kote nje ya makanisa na madhehebu:
Ufunuo 7:9,13,14 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kila kabila, na kila jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
Mungu Anaokoa kupitia kusikia neno la Mungu na si vinginevyo:
Warumi 10:17 Basi imani, huja kwa kusikia; na kusikia kwa neno la kristo.
Soma Biblia pamoja na nyumba yako yote (hasa na watoto); usomapo, omba rehema. Muombe Mungu wa Biblia mwenye rehema na neema akunusuru toka maangamizi yaliyo karibu kuja. Tunajifunza kidogo juu ya huruma ya Mungu katika kitabu cha Yona. Mungu pia aliwapa onyo waninawi kuhusu kuangamizwa kwa mji wao:
Yona 3:4-9 Mungu katika kitabu cha Yona. Mungu pia aliwapa onyo waninawi kuhusu kuangamizwa kwa mji wao: Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa ninawi wakamsadiki mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali ili msiangamizwe?
Mungu hakuwaangamiza waninawi. Ingawa hakuna uwezekano kwamba Mungu Hatakamilisha mpango Wake wa lengo la kuiangamiza dunia mwaka 2011, tunaweza kufahamu kuwa Mungu ni Mwenye huruma na Amejaa rehema. Jambo hili linabidi kututia moyo kila mmoja wetu kumwendea Mungu tukiomba rehema Yake kuu.

No comments:

Post a Comment